Aleksander Mashuhuri (Mkuu) | |
---|---|
Mfalme wa Masedonia | |
Aleksander jinsi alivyomshambulia mfalme Dario wa Uajemi kwenye mapigano ya Issos (mozaiki ya Aleksander mjini Napoli, Italia) | |
Kusimikwa | 336 |
Vyeo vingine | Mkuu wa shirikisho la Wagiriki, Shahanshah wa Uajemi, Farao wa Misri, Bwana wa Asia |
. | |
Wake | Roksana wa Baktria Stateira wa Uajemi Parysatis wa Uajemi |
Nasaba | Nasaba ya Masedonia |
Baba | Filipo II wa Masedonia |
Mama | Olimpia wa Epiros |
Aleksander Mashuhuri (au Aleksanda Mkuu, kwa Kigiriki Μέγας Αλέξανδρος, inayoandikwa kwa alfabeti yetu Megas Aleksandros) aliishi tangu Julai 356 KK hadi tarehe 11 Juni 323 KK.
Mfalme wa Masedonia (336 – 323 KK), anajulikana kama mmoja kati ya amiri jeshi waliofanikiwa kupita wote wengine katika historia ya dunia. Kabla hajafariki kwa umri wa miaka 33 aliteka sehemu kubwa ya dunia iliyojulikana na Wagiriki wa zamani zake, kuanzia Ulaya hadi Bara Hindi na Misri.