Amiri au Emir (ar. امير amīr au tur. emir) ni cheo cha mtawala mwislamu anayesimamia emirati. Kiasili maana yake ni "mwenye amri" kama cheo cha kijeshi au kiserikali.
Katika miaka ya kwanza ya Uislamu amiri alikuwa mkuu wa jeshi au sehemu ya jeshi. Baada ya kutwaa nchi alikuwa na nafasi kama gavana ya khalifa. Kutokana na upanuzi wa himaya ya kiislamu na ushaifu wa serikali kuu amiri aliweza kutawala mara nyingi kama mfalme mdogo lakini kwa kawaida alitafuta kibali cha khalifa.