Anasa (kutoka neno la Kiarabu) ni raha au starehe tele katika maisha ya binadamu.
Utafutaji wake mara nyingi unasababisha madhara kwake na kwa jamii, kuanzia afya ya mwili na ya nafsi, mbali ya maadili na maisha ya kiroho.
Ndiyo sababu dini mbalimbali zinahimiza kudhibiti tamaa na kuishi kwa adili la kiasi.