Anga-nje (kwa Kiingereza outer space) ni eneo la ulimwengu. Tofauti na anga ya dunia yetu inayojazwa na angahewa ni yote nje yake. Sehemu kubwa za anga za nje ni nafasi ambayo inakaribia hali yaombwe. Katika tupu hii kuna magimba ya angani kama sayari, nyota, galaksi, nebula na mawingu.
Wanasayansi hawaoni ya kwamba nafasi kati ya magimba ya angani ni hali ya ombwe au tupu kabisa lakini kuna kiasi kidogo cha utegili wa hidrojeni pamoja na mnururisho wa sumakuumeme na nyutrino. Katika nadharia ya fizikia kuna pia mata nyeusi na nishati nyeusi ambazo hazikuthibitishwa bado.