Antiokia wa Pisidia (kwa Kigiriki: Ἀντιόχεια τῆς Πισιδίας, Antiokeia tes Pisidias) ulikuwa mji wa Wagiriki wa Kale katika rasi ya Anatolia, sasa katika wilaya ya Isparta, nchini Uturuki.
Kwa sasa ni maghofu tu yanayopatikana km 1 kaskazini-mashariki kwa Yalvaç.
Mwaka 46 Mtume Paulo na Barnaba walifika mara mbili kuinjilisha huko (Mdo 13:13-52 na 14:21-23). Paulo alirudi tena katika maeneo hayo wakati wa safari yake ya pili (16:1) na ya tatu (18:23) ingawa alipatwa na dhuluma (2 Tim 3:11).