Jiji la Arusha | |
Mji wa Arusha na Mlima Meru | |
Majiranukta: 03°22′S 36°41′E / 3.367°S 36.683°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Arusha |
Wilaya | Arusha |
Kata | 25 |
Mitaa | 155 |
Serikali[1] | |
- Aina ya serikali | Halmashauri ya Jiji |
- Mstahiki Meya | Maximilian Matle Iranqe |
- Kaimu Mkurugenzi wa Jiji | Hargeney Reginald Chitukuro |
Eneo | |
- Jumla | 267 km² |
Mwinuko | 1,457 m (4,777 ft) |
Idadi ya wakazi (2022)https://www.nbs.go.tz | |
- Wakazi kwa ujumla | 617,631 |
- Mtawanyiko wa watu | 1,560/km² (4,040.4/sq mi) |
EAT | (UTC+3) |
Msimbo wa posta | 231xx |
Kodi ya simu | 027 |
Tovuti: Halmashauri ya Jiji la Arusha |
Arusha ni jiji lililomo kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Ina postikodi namba 23100.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442.[2]: 26 Mwaka 2022 walihesabiwa 617,631 [3].
Mji huo upo kando ya Mlima Meru kwenye ncha ya mashariki mwa Bonde la Ufa na umezungukwa na baadhi ya mandhari maarufu barani Afrika zikiwa pamoja na mbuga za wanyama. Hifadhi ya Arusha, Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti na Ngorongoro, Ziwa Manyara, Olduvai Gorge, Hifadhi ya Tarangire na mlima Kilimanjaro vipo karibu na mji huu.
Mji huu umezungukwa na milima kaskazini na mashariki, na mazingira yake ni mchanganyiko wa misitu ya savanna na misitu mabaki. Hali ya hewa ni nzuri sana.
Hadi sasa ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa.
<ref>
tag; no text was provided for refs named ArushaCC
<ref>
tag; no text was provided for refs named Sensa_2012