Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Bahari ya Aktiki

Ramani ya Bahari ya Aktiki
Dubu nyeupe huishii katika eno la Aktiki

Bahari ya Aktiki (Aktika) ni bahari inayozunguka ncha ya kaskazini. Ni sehemu ya eneo la Aktiki. Wataalamu wengine huitazama kama bahari ya pekee lakini wengine huona ni bahari ya pembeni ya Atlantiki. Kina kikubwa kiko karibu na visiwa vya Spitzbergen chenye mita 5,608.

Bahari ya Aktiki iko kati ya pwani za Asia ya Kaskazini, Alaska na Kanada katika Amerika ya Kaskazini, Greenland na Skandinavia (Ulaya). Eneo lake ni 14.056 km². Kati ya Greenland na Skandinavia kuna uwazi kubwa unaojifungua kwa Atlantiki ya Kaskazini na mlango wa Bering unaunganisha bahari hii na Pasifiki.

Sehemu kubwa ya eneo lake hufunikwa na barafu yenye unene wa mita 3 lakini sehemu hii imeanza kupungua kutokana na kupanda kwa halijoto duniani.

Mito muhimu inayoingia ni Ob, Yenissei, Lena na Kolyma upande wa Siberia (Urusi) halafu mito ya Yukon na Mackenzie upande wa Amerika ya Kaskazini.


Previous Page Next Page