Bahari ya Flores (kwa Kiingereza: Flores Sea) ni sehemu ya bahari kati ya visiwa vya Indonesia.
Inapakana na kisiwa cha Celebes (Sulawesi) upande wa kaskazini. Visiwa vya Flores na Sumbawa viko upande wa kusini vikitenganisha sehemu hii na Bahari Hindi[1].
Eneo lake ni kilomita za mraba 240,000.