Bahari ya Kaspi (Kiarabu: بحر قزوين Baḥr Qazvin; Kiajemi: دريا خزر darya khazar; Kirusi: Каспийское море kaspiiskoye more) ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371,000 na mjao wa km³ 78,200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.
Kimo chake kinafikia mita 1,025.
Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.