Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Bahari ya Maluku

Mahali pa Bahari ya Maluku.
Bahari ya Maluku.

Bahari ya Maluku (kwa Kiingereza: Moluccan Sea) ni sehemu ya Bahari ya Pasifiki, ndani ya nchi ya Indonesia. Ni eneo lenye miamba tumbawe mingi na nafasi nzuri ya kupiga mbizi.

Bahari ya Maluku inapakana na Bahari ya Banda upande wa kusini na Bahari ya Celebes upande wa kaskazini.

Iko kati ya visiwa vya Maluku na Sulawesi (Celebes). Visiwa vya Talaud kaskazini ndivyo mwisho wa bahari hiyo.

Eneo lake ni takriban kilomita za mraba 200,000. Kina cha maji hufikia mita 4,810.

Chini ya bahari hii mabamba ya gandunia husukumana na hivyo kusababisha matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.


Previous Page Next Page