Balbu (pia: globu; kutoka Kiing. light bulb au light globe) ni kifaa cha kutolea nuru ikiwashwa yaani wakati umeme unapitishwa ndani yake. Hutumiwa kama sehemu ya kifaa kikubwa zaidi kama taa ya umeme.
Balbu hufanya kazi yake kwa kipindi fulani tu baadaye inakwisha inahitaji kubadilishwa. Wakati wa kutoa nuru inashika joto na kwa balbu zenye uzi joto hii huwa na kiwango cha kumwumiza mtu anayeigusa. Ikibadilishwa ni lazima kuangalifu maana inawezekana kupigwa na umeme kama mtu anagusa soketi yaani upande wa taa inayoshika balbu.