Bangi (pia: bhang, bhangi kutoka Kihindi भांग, bhāṅg) ni majani ya mmea wa kike wa mbangi (Cannabis). Ndani yake mna dawa inayosababisha namna ya ulevi unaotegemea kiasi cha dawa kinachoingia mwilini. Hata hivyo ina uwezo wa hali ya juu kukabiliana na magonjwa sugu kama vile kansa, kusaidia mgonjwa mwenye maumivu makali sana na kuongeza hamu ya kula kwa mgonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI). Pia bangi ina saidia kusawazisha kiwango cha presha
Hutumika pia kwa mapishi pamoja na maua (matumba). Hutumika aidha kama kinywaji, kama kiungo ndani ya vyakula au huvutwa.