Bao (au Bao la Kiswahili au Bao la Zanzibar) ni mchezo wa jadi wa aina ya mankala unaochezwa na wachezaji wawili.
Mchezo wa Bao umesambaa sana katika nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania Bara (Tanganyika), Zanzibar na Kenya, lakini pia Rwanda, Komori, Malawi[1] pamoja na baadhi ya maeneo ya DR Congo na Burundi.
Nchini Tanzania, hasa Zanzibar, wachezaji wanashindana mara kwa mara na washindi wanaitwa mabingwa, lakini pia mafundi, wasanii na wanaheshimiwa sana.
Jina lenyewe "Bao" ni neno la Kiswahili kwa "ubao" au "mchezo wa ubao".
Bao ni mchezo mgumu kuliko michezo yote ya aina ya mankala. Inajulikana sana kuwa mancala mashuhuri katika suala la utata na kina kimkakati, [2] na imeibua shauku kwa wasomi wa taaluma kadhaa, ikijumuisha nadharia ya mchezo, nadharia changamano, na saikolojia.[3]
Nje ya Afrika watalaamu wa michezo na wanasaikolojia wanavutiwa sana na mchezo huu.
Mashindano rasmi yanafanyika Tanzania, Zanzibar, Lamu (Kenya), na Malawi, na Tanzania Bara na Zanzibar zote zina vyama vyao vya Bao, kama vile Chama cha Bao kilichoanzishwa mwaka wa 1966.
Aina nyingine za Bao ni Sono ya Wagogo, Engesho ya Wamasai, n.k.