Baraza la mawaziri ni baraza linaloongoza tawi la utendaji la serikali. Wanachama wa baraza huitwa mawaziri ama makatibu, k.m. Kenya na Marekani.
Kazi ya baraza la mawaziri inatofautiana kulingana na nchi: katika baadhi ya nchi, ni kikundi kilicho na wajibu wa kufanya maamuzi kwa pamoja, kwingine, linaweza kuwa kikundi cha washauri au wasaidizi katika kufanya maamuzi kwa mkuu wa nchi au mkuu wa serikali. Baraza la mawaziri huwa na wajibu wa usimamizi wa kila siku wa shuguli za serikali.
Waziri huwa na jukumu la kutawala wizara, au idara Marekani. Pia, mawaziri huwa waanzilishi wazuri na muhimu wa miswada bungeni.
Sehemu ya mfululizo wa serikali kuhusu |
Utendaji |
---|
Mkuu wa Nchi |
Serikali |
Baraza la Mawaziri |
|
Mifumo |