Bendera ya Burkina Faso ina milia miwili ya kulala ya nyekundu na ya kijani. Katikati iko nyota ya pembetano ya rangi njano.
Hizi rangi za nyekundu-kijani-njano ni rangi za Umoja wa Afrika.
Bendera hii ilianzishwa rasmi Agosti 1984.
Kabla ya tarehe hii Burkina Faso ilitumia bendera ya zamani iliyoanzishwa 1960 wakati wa uhuru wa "Volta ya Juu".