Bendera ya Jamhuri ya Kongo ina milia mitatu ya hanamu yenye rangi za Umoja wa Afrika kijani-njano-nyekundu.
Ilianzishwa Agosti mwaka 1958 Kongo ilipopata madaraka ya kujitawala ndani ya Umoja wa Kifaransa ikaendelea kuwa bendera ya taifa baada ya uhuru kamili mwaka 1960.
Mwaka 1970 wakati wa Jamhuri ya Watu wa Kongo bendera ilibadilishwa kuwa bendera nyekundu yenye nyota na jembe pamoja na nyundo za njano halafu majani ya mnazi ya kijani.
Wakati wa kuporomoka kwa itikadi ya kikomunisti na kisoshalisti serikali ya rais Denis Sassou-Nguesso ilirudisha bendera ya zamani mwaka 1991.