Binamu ni ndugu wa ukoo tofauti, kwa sababu ni mtoto wa mjomba au wa shangazi, si mtoto wa baba mkubwa, baba mdogo, mama mkubwa wala mama mdogo (ingawa kwa Kiingereza hao wote wanaitwa "cousins").
Kuhusu mahusiano na uwezekano wa kuoana kuna desturi na sheria tofauti duniani.