Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Borno (jimbo)

Wacheza ngoma, Borno
Faili:Nigeria-Borno ramani.PNG
Ramani ya Borno

Borno ni jimbo la Nigeria katika kaskazini ya nchi lenye wakazi milioni nne na nusu. Mji mkuu pia mji mkubwa wa jimbo ni Maiduguri (wakazi 1,112,511).

Imepakana na nchi jirani za Niger, Chadi na Kamerun, halafu majimbo ya Nigeria ya Adamawa, Yobe na Gombe.

Borno ni hasa eneo la Wakanuri. Jimbo la leo ni mabaki ya milki ya Bornu ya karne zilizopita. Milki hii ya Kanem-Bornu ilitawala eneo kubwa katika mazingira ya Ziwa Chadi kwa muda wa miaka 600 tangu mnamo 1300. Milki iliporomoka mwisho wa karne ya 19 na amiri yake ya mwisho aliuawa na Mwarabu Rabih az-Zubayr kutoka Sudan. Baada ya Wafaransa chini kumshinda Zubayr mwaka 1900 eneo la Bornu likagawiwa na nchi za Ulaya. Sehemu kubwa likawa chini ya Uingereza, na maeneo mengine chini ya Ufaransa na Ujerumani. Waingereza walirudishwa familia ya watawala wa Borno kwa cheo cha amiri wa Borno.

Katika Nigeria huru Bornu iliingizwa katika jimbo la Kaskazini-Mashariki lililogawiwa 1976. Jimbo kubwa la Borno likagawiwa tena kwa kutenga jimbo la Yobe.

Hadi leo amiri wa Borno ana athira kubwa katika siasa hata kama hana cheo cha kiserikali tena bali ya kiutamaduni tu.


Previous Page Next Page






Bọrọnu ANN برنو (ولاية) Arabic Borno ştatı AZ بورنو ایالتی AZB Борно Bulgarian Borno State BI Borno (Nigeria) BR Estat de Borno Catalan Borno State CEB Borno Czech

Responsive image

Responsive image