Bustani ya wanyama ni mahali ambapo wanyama, hasa wanyamapori wa aina mbalimbali, wanatunzwa ili watu wapate kuwatazama. Siku hizi bustani Za wanyama zimekuwa pia mahali pa kutunza spishi au aina za wanyama walioko hatarini kutokomea. Vile vile bustani za wanyama zimewekwa kwa ajili ya maonyesho[1].
Miji mingi mikubwa duniani ina bustani za wanyama[2]. Katika baadhi ya bustani hizo watu hulipa kiingilio wakitaka kuingia. Hata hivyo bustani hizo hazipokei mapato ya kutosha, hivyo hazina budi kupokea pia misaada kutoka serikali.
Umuhimu wa bustani za wanyama ni katika