Buti (wingi: mabuti; kutoka Kiingereza "boot") ni aina ya kiatu kikubwa kinachofunika mguu pengine hadi magotini. Mara nyingi huwa la ngozi, lakini yale ya kisasa hufanywa kutoka kwa vifaa mbalimbali.
Buti huvaliwa kwa kazi maalumu - kulinda mguu kutokana na maji, baridi kali, matope au hatari (kwa mfano, kutokana na kemikali au kutumia vidole vya chuma) au kutoa usaidizi wa ziada wa mguu kwa shughuli zenye nguvu au kwa sababu ya mtindo .
Katika hali nyingine, kuvaa buti kunahitajiwa na sheria au kanuni, kama katika baadhi ya mamlaka zinazohitaji wafanyakazi katika maeneo ya ujenzi kuvaa mabuti ya chuma. Buti linashauriwa pia kwa wapanda pikipiki.