Jiji la Cape Town | |||
| |||
Mahali pa mji wa Cape Town katika Afrika Kusini |
|||
Majiranukta: 33°55′48″S 18°27′36″E / 33.93000°S 18.46000°E | |||
Nchi | Afrika Kusini | ||
---|---|---|---|
Majimbo | Rasi Magharibi | ||
Tovuti: www.capetown.gov.za |
Cape Town (yaani "Mji wa rasi", kwa Kiafrikaans: Kaapstad; kwa Kixhosa: iKapa) ni mji mkubwa wa tatu wa Afrika Kusini na mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya nchi ikiwa ni makao ya Bunge. Pia ni mji mkuu wa jimbo la Rasi Magharibi (Western Cape / Wes-Kaap). Ni sehemu ya Jiji la Cape Town.
Eneo lake ni km² 1,644 lenye wakazi 2,375,910 (mwaka 2005).
Jina la mji limetokana na Rasi ya Tumaini Jema iliyoko karibu na mji upande wa kusini.