Chato ni kata ya Wilaya ya Chato katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Msimbo wa posta ni 30301. [1]
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 25,771 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,508 waishio humo.[3]
Chato imekuwa maarufu hasa kama asili ya rais John Magufuli ambaye amekuwa mbuge wa Chato kwa miaka 25, na ameitoa Chato kutoka katika kijiji miaka ya 2000 hadi kuwa wilaya kubwa yenye shule, miundombinu mizuri.
Wakati wa uongozi wake kama rais alielekeza huko pesa nyingi za umma kuiendeleza kwa kila namna, kama vile kuwezesha ujenzi wa standi ya mabasi ya kisasa (japo ilikuwa programu ya nchi nzima), hospitali ya kanda, hoteli ya kitali na uwanja wa ndege wa tatu kwa ukubwa nchini. [4].