Chuma cha pua (pia: chumapua, feleji) ni aloi wa chuma pamoja na gredi mbalimbali za kaboni ambayo imekuwa uti wa mgongo wa mapinduzi ya viwandani. Hadi leo ni msingi wa mashine na vifaa vingi, pia silaha zinazounda uwezo wa kijeshi wa mataifa. Pia ujenzi wa kisasa hauwezekani bila chuma cha pua.
Chuma cha pua ni ngumu kushinda chuma tupu isiyo na kaboni. Siku hizi kuna pia aloi za chumapua ambamo dutu tofauti na kaboni hutumiwa.