Dola ya Kanada (alama: $; msimbo: CAD; Kifaransa: dollar canadien) ni sarafu ya Kanada. Inafupishwa kwa alama ya dola $. Hakuna muundo wa kawaida wa kutofautisha, lakini vifupisho kama Can$, CA$, na C$ hutumiwa mara kwa mara kutofautisha na sarafu nyingine zinazotumia dola (ingawa C$ inaweza kuchanganyikiwa na córdoba ya Nikaragua). Inagawanywa katika senti 100 (¢).