Dunia | |
---|---|
Jina | |
Asili ya jina | Kar. دنيا, (dunyaa) |
Majina mengine | Ardhi, nchi |
Alama | |
Tabia za mzunguko | |
Mkaribio | km 147,098,450 au 0.983292 |
Upeo | km 152,097,597 au 1.01671 |
km 149,598,023 au 1.0 | |
Uduaradufu | 0.0167086 |
siku 365.256363004 | |
Mwinamo | 0.00005° toka njia ya Jua |
Miezi | Mwezi |
Tabia za maumbile | |
km 6371.0 | |
Tungamo | kg 5.972168×1024 |
g/cm3 5.5134 | |
Uvutano wa usoni | m/s2 9.80665 |
siku 1.0 | |
siku 0.99726968 | |
Weupe | 0.306 (Bond) 0.367 (jiometri) |
Halijoto | K 287.91 (14.76°C) |
Dunia ni kiolwa cha angani ambapo juu yake tunaishi sisi binadamu na viumbehai wengine wengi, tukipata mahitaji yetu, kuanzia hewa ya kutufaa na maji.
Dunia ni mojawapo ya sayari nane zinazozunguka Jua letu katika anga-nje. Kati ya sayari za Mfumo wa Jua, Dunia yetu ni sayari ya tatu kutoka kwa Jua.
Masafa baina yake na Jua ni kilomita milioni 150 au kizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka Jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756.
Umri wa Dunia hukadiriwa kuwa miaka bilioni 4.5[1][2].
Ni mahali pekee katika ulimwengu panapojulikana kuna uhai ulioaminiwa kuanza miaka bilioni 3.5 iliyopita[3].
Uhai unapatikana kwa spishi milioni 10-14 za viumbe hai pamoja na wanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7.2[4].