Eldoret | |
Mahali pa mji wa Eldoret katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°31′0″N 35°17′0″E / 0.51667°N 35.28333°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Uasin Gishu |
Idadi ya wakazi (2009) | |
- Wakazi kwa ujumla | 289,380 |
Eldoret ni mji ulio magharibi mwa Kenya. Upo kwenye barabara kuu kati ya Nairobi - Kampala takriban km 300 kutoka jiji la Nairobi katika nyanda za juu magharibi mwa Bonde la Ufa kwenye kimo cha mita 2100 - 2700 juu ya UB.
Ukiwa na wakazi 289,380 (wakati wa sensa ya mwaka 2009[1]) ni mji wa tano kwa ukubwa nchini Kenya baada ya Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru na ni makao makuu ya kaunti ya Uasin Gishu.