Emirati (kutoka Kiarabu: إمارة) ni nchi inayotawaliwa na emir au amiri ambaye ni mtawala kama mtemi anayerithi cheo chake kama mfalme lakini cheo hicho hutazamwa si sawa na mfalme.
Jina hilo lenye asili ya Kiarabu ni kawaida katika utamaduni wa Kiislamu. Falme za Kiarabu zinajiita "emirati" kwa lugha ya Kiarabu.
Wakati mwingine neno hilo linataja sehemu ya nchi tu kama inaongozwa na mtu wa familia ya kifalme wa nchi mwenye cheo cha amiri, kama mikoa ya Saudia.
Katika historia watawala wa emirati kadhaa walibadilisha cheo chao kuwa mfalme au sultani.