Frankfort | |
Mahali pa mji wa Frankfort katika Marekani |
|
Majiranukta: 38°11′50″N 84°51′47″W / 38.19722°N 84.86306°W | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | Kentucky |
Wilaya | Franklin |
Idadi ya wakazi (2000) | |
- Wakazi kwa ujumla | 27,741 |
Tovuti: www.CityofFrankfortKY.com |
Frankfort ni jina la mji mkuu wa jimbo la Kentucky nchini Marekani. Umepata kuwa mji mkuu tangu mnamo tar. 8 Desemba 1792. Mji huu upo nga'mbo ya Mto Kentucky. Hii ndiyo sababu iliyopelekea mji huu kuitwa jina hili, kwa sababu ardhi yake ilikuwa ikimilikiwa na mwanzilishi Stephen Frank. Awali uliitwa "Frank's Ford", lakini baada ya muda mchache jina likabadilishwa na kuwa Frankfort. Takriban watu 27,741 wanaishi mjini hapa. Na huu ni mji mkuu wa tano kwa udogo katika orodha ya miji mikuu ya majimbo ya Marekani.