Garissa | |
Mahali pa mji wa Garissa katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°27′25″S 39°39′30″E / 0.45694°S 39.65833°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Garissa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 119,696 |
Garissa ni mji nchini Kenya ulio makao makuu ya kaunti ya Garissa. Unaunda kata ya eneo bunge la Garissa Mjini[1].
Wakazi walikuwa 119,696 wakati wa sensa ya mwaka 2009[2].
Mto Tana hupitia eneo la manispaa.
Wakazi walio wengi ni raia wa Kenya walio Wasomali kwa lugha na utamaduni pamoja na raia wa Somalia waliohamia hapa kutokana na hali ya vita nchini mwao. Kundi kubwa la wenyeji ni wa ukoo wa Waogaden.