George H. W. Bush | |
Makamu wa Rais | Dan Quayle |
---|---|
mtangulizi | Ronald Reagan |
aliyemfuata | Bill Clinton |
tarehe ya kuzaliwa | 12 Juni 1924 |
ndoa | Barbara Pierce (1945-2018) |
watoto | George W. Bush, rais wa 43 wa Marekani |
signature | |
tovuti | Presidential Library |
George Herbert Walker Bush ( 12 Juni 1924 - 30 Novemba 2018) alikuwa Rais wa 41 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1989 hadi 1993. Kaimu Rais wake alikuwa Dan Quayle.
Akijulikana kama George Bush aliwahi kuwa mbunge, balozi wa Marekani, mkuu wa mamlaka ya upelelezi CIA na makamu wa rais Ronald Reagan. Alikuwa mwanasiasa wa Chama cha Jamhuri cha Marekani (Republican).
Kipindi cha urais wa Bush kiliona kuporomoka kwa ukomunisti katika Urusi na Ulaya ya Mashariki na mwisho wa vita baridi. Alitafuta maelewano na viongozi wa Urusi na kukubali maungano ya Ujerumani. Alituma jeshi la Marekani kwenye uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliompindua dikteta Manuel Noriega na kwenye vita dhidi ya Irak iliyowahi kushambulia Kuwait.
Mwana wake George Walker aliingia pia katika siasa akaendelea kuwa rais wa 43 wa Marekani.