Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Gesi adimu

Gesi adimu ni mfulizo wa kikemia katika mfumo radidia unaounganisha elementi za kundi la 18 yaani Heli (He), Neoni (Ne), Arigoni (Ar), Kriptoni (Kr), Zenoni (Xe) na Radoni (Rn).

Elementi hizi zote zapatikana kama gesi kwa hali sanifu; hazina rangi wala harufu; haziwaki.

Zinapatikana katika hali ya atomu pekee, si kama molekuli. Hazimenyuki yaani haziungani na atomu yingine kuwa molekuli. Sababu ya kutomenyuka ni tabia ya mzingo elektroni wa nje kujaa kabisa; hapa mzingo elektroni wa nje huwa na idadi ya elektroni inayowezekana tofauti na elementi nyingi ambako mzingo elektroni wa nje ina idadi ya elektroni ambayo ni chini ya idadi ya nafasi zake. Kwa hiyo hakuna haja kutafuta hali thabiti zaidi; gesi hizi zimeshafikia hali thabibiti kila atomi peke yake. Hivyo hakuna kampaundi za gesi hizi.

Gesi hizi zote ziko hewani lakini kwa kiasi kidogo tu. Radoni pekee yake ni hatari ya binadamu lakini si kwa sababu ya tabia zake za kikemia bali na tabia yake ya kifizikia kwa sababu radi ni elementi mnururishi.


Previous Page Next Page






Edelgasse AF Gas noble AN غاز نبيل Arabic غاز نبيل ARY Gas noble AST Təsirsiz qazlar AZ نجیب قاز AZB Затлы газдар BA Gas mulia BAN Інертныя газы BE

Responsive image

Responsive image