Golikipa (kutoka Kiingereza "goalkeeper"; pia kipa tu; kwa jina lingine mlinda lango) ni mchezaji maalumu ambaye hulinda lango la timu katika michezo mingi kama soka na hockey inayohusisha kufunga katika lango.
Kazi ya kipa ni kuzuia timu pinzani kufunga bao kwa kuingiza mpira golini. Yaani yeye anayepewa jukumu la kuzuia timu pinzani kufunga goli katika lango lake.
Nafasi hii ni mahususi katika michezo ya Soka, bandy, rink bandy, camogie, Gaelic football, Mpira wa sakafu, mpira wa mikono, hockey, polo na michezo mingine mingi.
Katika michezo mingi inayohusisha kufanga katika wavu, sheria maalumu huwekwa kwa mlinda lango tofauti na wachezaji wengine. Sheria hizo hulenga kunlinda golikipa dhidi ya hatari na vitendo vyenye athari kwake.
Hii inaweza kuonekana sanasana katika mchezo wa hokey ambapo golikipa huvaa mavazi maalumu kama kofia ngumu ili kumlinda na vishindo kutokana na kugongwana vitu vigumu kama fimbo ya kuchezea na mpira.
Baadhi ya michezo, golikipa hufuata sharia kama wachezaji wengine, mfanoi, katika mchezo wa soka, anaweza kupiga mpira kwa miguu kama wachezaji wengine, lakini pia anaweza kutumia mikono yake ila kwenye eneo maalumu tu. Baadhi ya michezo golikipa hana uhuru wa kucheza uwanja mzima, na baadhi ya matendo hawezi kufanya akiwa nje ya eneo linaloruhusiwa.