Grife (ing. slate) ni mwamba metamofia. Imeundwa kutoka kwa mwambatope iliyoathiriwa na shinikizo kubwa na joto. Mwambatope wenyewe ni mwamba mashapo unaotokana na matope ya udongo wa mfinyanzi ukipasuka kirahisi kwa bapa nyembamba. Tabia hiyo ya kupasuliwa kirahisi inaendelea katika grife kwa kuwa chini ya shinikizo na joto la wastani.