Jamhuri ya Gine | |
---|---|
République de Guinée (Kifaransa) Hawtaandi Gine (Kipular) ߖߌ߬ߣߍ߫ ߞߊ ߝߊߛߏߖߊߡߊߣߊ (Kimaninka) | |
Kaulimbiu ya taifa: Travail, Justice, Solidarité (Kifaransa) "Kazi, Haki, Mshikamano" | |
Wimbo wa taifa: Liberté (Kifaransa) "Uhuru" | |
Mahali pa Guinea | |
Ramani ya Guinea | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Conakry |
Lugha rasmi | Kifaransa |
Gine (pia: Gini; kwa Kifaransa: Guinée; kwa Kiingereza: Guinea; jina rasmi Jamhuri ya Gine) ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Gine-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Gine-Bisau na Gine ya Ikweta.
Imepakana na Gine-Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi.
Eneo lake ni chanzo ya mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia.