Haile Selassie (kwa Kige'ez: ቀዳማዊ ኃይለ ሥላሴ, qädamawi haylä səllasé, [ˈhaɪlə sɨlˈlase]; 23 Julai 1892 – 27 Agosti 1975) alikuwa Kaisari au Negus Negeste wa Ethiopia. Kabla ya kuwa mfalme aliitwa Ras Tafari Makonnen. Jina lake la kifalme lina maana ya "Utukufu wa Utatu (Mtakatifu)". Pia anafahamika kwa jina la Simba wa Yuda, Mfalme wa wafalme.
Alikuwa Mkristo, tena shemasi wa madhehebu ya Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia.