Hidalgo ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kati ya nchi. Imepakana na San Luis Potosí, Veracruz, Puebla, Tlaxcala, Mexico na Querétaro. Mji mkuu na mji mkubwa ni Pachuca.
Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 2,345,514. Una eneo la 20,502 km².
Jina la jimbo lilitolewa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru wa Mexiko Miguel Hidalgo y Costilla.
Gavana wa jimbo ni Miguel Ángel Osorio Chong.
Lugha rasmi ni Kihispania.