21°27′27.20″N 39°51′33.90″E / 21.4575556°N 39.8594167°E
Hira (kwa Kiarabu: حراء Ḥirāʾ) au Pango la Hira (غار حراء Ġār Ḥirāʾ) ni pango lililopo karibu na mji wa Makka, kwenye Jabal an-Nūr, kanda ya Hejaz ya Saudi Arabia ya leo. Pango peke yake lina eneo la m 4 na urefu wa m 1.75 kwa mapana[1].
Linafahamika zaidi na Waislamu kwa kuwa sehemu ambao mtume Muhammad amepokea aya ya kwanza kutoka kwa Mwenyezi Mungu (Allah) kupitia malaika wake Jibril[1].