| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: sawa na China | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | -- Kihistoria makao ya serikali ilikuwa Victoria City. | ||||
sehemu yenye wakazi wengi | wilaya ya Sha Tin | ||||
Lugha rasmi | · Kichina (lahaja ya Kanton) Kiingereza | ||||
Serikali | John Lee | ||||
Ilianzishwa Kutwaliwa na Uingereza |
25 Januari 1841 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,104 km² (--) 4.58 | ||||
Idadi ya watu - 2014 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
7,234,800 (ya 100) 6,708,389 6,544/km² (ya 3) | ||||
Fedha | Hong Kong dollar (HKD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
HKT (UTC+8) {{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}}) | ||||
Intaneti TLD | .hk | ||||
Kodi ya simu | +852 (01 from Macau)
- |
Hong Kong (kwa Kichina: 香港) ni eneo lenye utawala wa pekee ndani ya Jamhuri ya Watu wa China.
Iko upande wa mashariki wa delta ya Mto Zhu Jiang (Pearl River, Mto Lulu) unapoishia katika Bahari ya Kusini ya China. Inatazama bahari ya Uchina upande wa kusini ikipakana na jimbo la Guangdong upande wa kaskazini. Tarehe 23 Oktoba 2018 rais wa China Xi Jinping alizindua rasmi daraja la baharini refu kuliko yote duniani (kilometa 55) linalounganisha Hong Kong, Macau na China bara (mji wa Zhuhai).
Hongkong ilikuwa koloni la Uingereza kwenye pwani ya China kwa zaidi ya miaka 99, likarudishwa chini ya utawala wa Kichina mwaka 1997. Inaendelea kutawaliwa na sheria zake za pekee chini ya mamlaka kuu ya serikali ya Beijing.
Siku hizi ni eneo tajiri kabisa katika Uchina wote.