Isimujamii (pia isimu jamii; kwa Kiing. sociolinguistics) ni tawi la isimu (taaluma inayochunguza lugha kisayansi) ambalo huchunguza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.
Aidha inajihusisha na athira yeyote ya jamii kama vile desturi za watu, matazamio, na muktadha, katika nyanja za lugha namna inavyotumika.
Chini ya taaluma hiyo, kuna matawi mengi yanayoshughulikia uchanganuzi wa vipengele fulani vya uhusiano kati ya lugha na jamii, k.m.
- uhusiano kati ya lugha na utamaduni
- matumizi ya aina tofauti za lugha na mazingira yake, kama lahaja, rejista na mtindo
- matumizi ya lugha tofauti wakati mmoja, kama katika wingilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia
- vipengele mbalimbali vya mawasiliano kupitia maoni ya msemaji (tawi hilo pia huitwa isimu amali)
- matumizi ya lugha baina ya jamii za watu tofauti, kama lugha mawasiliano, pijini na krioli
- uhusiano kati ya lugha na siasa katika upangaji lugha na sera za lugha
- Uhusiano kati ya lugha na maendeleo ya jamii( kiuchumi, kisayansi n.k)