Kata ya Itumba | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Songwe |
Wilaya | Ileje |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 10,566 |
Itumba ni kata ya Wilaya ya Ileje na ndiyo makao makuu ya wilaya hiyo. Imepakana na Isongole ambayo imepakana na nchi ya Malawi katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53401.
Jina linatokana na tumbaku kwa lugha ya Kilambya. Hii ni kwa sababu mtawala mkuu wa Walambya alikuwa analima tumbaku pembezoni mwa mto Itumba, nayo ilikuwa inastawi sana pembezoni mwa mto huo.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,566 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata hii ilikuwa na wakazi wapatao 10,186 [2] walioishi humo.