| |||||
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: Денес над Македонија Leo juu ya Masedonia | |||||
Mji mkuu | Skopje (tamka: "skopye" | ||||
Mji mkubwa nchini | Skopje | ||||
Lugha rasmi | Kimasedonia1 | ||||
Serikali | Jamhuri ya kibunge Gordana Siljanovska-Davkova (Гордана Сиљановска-Давкова) Hristijan Mickoski (Христијан Мицкоски) | ||||
Independence Ilitangazwa |
8 Septemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
25,333 km² (ya 148) 1.9 | ||||
Idadi ya watu - 2011 kadirio - Msongamano wa watu |
2,058,539 (ya 146) 80.1/km² (ya 122) | ||||
Fedha | Denar ya Masedonia (MKD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .mk | ||||
Kodi ya simu | +389
- | ||||
1Kimasedonia ndiyo lugha rasmi pamoja na Kialbania. Kila lugha inayotumiwa na 20% ya wakazi hutumiwa kama lugha rasmi ya nyongeza kimahali kama vile Kituruki, Kiromany na Kiserbia. |
Jamhuri ya Masedonia Kaskazini (jina jipya lililoanza kutumika mnamo Februari 2019; kwa Kimasedonia: Република Северна Македонија, Republika Severna Makedonija; kwa Kialbania: Republika e Maqedonisë së Veriut) ni nchi kwenye rasi ya Balkani katika Ulaya ya kusini mashariki. Imepakana na Serbia, Albania, Ugiriki na Bulgaria.
Mji mkuu ni Skopje, wenye wakazi 600,000. Miji midogo zaidi ni pamoja na Bitola, Prilep, Tetovo, Kumanovo, Ohrid, Veles, Štip, Gostivar na Strumica.
Masedonia Kaskazini ni nchi mwanachama ya Umoja wa Mataifa na inasubiri kupokewa katika Umoja wa Ulaya.