Jiografia ni somo la Dunia na vipengele vyake, wakazi wake, na maajabu yake.[1]
Neno la Kiswahili jiografia linafuata matamshi ya Kiingereza ya neno la Kigiriki "γεωγραφία", geo-grafia kutoka gê "dunia" na graphein "kuandika". Lina maana ya "kuandika kuhusu Dunia". Neno hili lilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasayansi Eratosthenes (276-194 KK).
Sehemu za jiografia ni vitu kama mabara, bahari, mito na milima. Wakazi wake ni watu wote na wanyama waishio juu yake. Maajabu yake ni vitu vinavyotokea kama vile maji kujaa na kupwa, upepo, na tetemeko la ardhi.