Jiwe mchanga (kwa Kiingereza: sandstone) ni aina ya mwamba mashapo. Linaundwa na mchanga uliogandamizwa, hivyo madini ndani yake ni hasa shondo na felispa.
Jiwe mchanga ni mwamba thabiti ambayo hailikwi kirahisi, pia si ngumu mno, hivyo hutumiwa kwa ujenzi katika nchi nyingi.
Jiwe mchanga linabadilika kuwa kwasiti kama inaathiriwa na shinikizo kubwa, kwa mfano chini ya matabaka ya ardhi au kama linalala chini ya milima.