John Samwel Malecela (amezaliwa tar. 20 Aprili 1934). Alikua mbunge wa jimbo la Mtera katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania.[1] Anatokea katika chama cha CCM. Pia alikua Naibu Mwenyekiti wa CCM kuanzia mwaka (2005-2009), Waziri Mkuu (1990-1994), Kamishina Mkuu wa Tanzania huko Uingereza (1989-1999), Waziri wa Utamaduni Chakula na Usalama (1975-1980), na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (1972-1975).