Mwalimu Julius Nyerere | |
Muda wa Utawala 26 Aprili 1964 – 5 Novemba 1985 | |
Waziri Mkuu | Rashidi Kawawa (1972–77) Edward Sokoine (1977–80) Cleopa Msuya (1980–83) Edward Sokoine (1983–84) Salim A. Salim (1984–85) |
---|---|
Makamu wa Rais | Abeid Karume (1964–72) Aboud Jumbe (1972–84) Ali Hassan Mwinyi (1984–85) |
aliyemfuata | Ali Hassan Mwinyi |
Rais wa Tanganyika
| |
Muda wa Utawala 9 Desemba 1962 – 25 Aprili 1964 | |
Waziri Mkuu | Rashidi Kawawa |
Waziri Mkuu wa Tanganyika
| |
Muda wa Utawala 1 Mei 1961 – 22 Januari 1962 | |
Monarch | Elizabeth II |
mtangulizi | Ofisi iliundwa |
aliyemfuata | Rashidi Kawawa |
Waziri Kiongozi wa Tanganyika
| |
Muda wa Utawala 2 Septemba 1960 – 1 Mei 1961 | |
Monarch | Elizabeth II |
tarehe ya kuzaliwa | Butiama, Tanganyika | 13 Aprili 1922
tarehe ya kufa | 14 Oktoba 1999 (umri 77) London, Uingereza |
mahali pa kuzikiwa | Butiama, Tanzania |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
ndoa | Maria Nyerere |
watoto | 7 |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Makerere Chuo Kikuu cha Edinburgh |
Fani yake | Mwalimu |
dini | Ukristo (Katoliki) |
tovuti | juliusnyerere.info |
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, Mkoa wa Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 - London, Uingereza, 14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo.
Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.
Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."
Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi.
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma lilianza kushughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia "mtumishi wa Mungu". Baada ya hapo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limepokea jukumu la kuratibu mchakato huo pamoja na kesi kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kutokana na Nyerere kuishi muda mrefu jijini humo[1].