Karate (pia kareti, kutoka Kijapani: 空手) ni aina ya michezo ya mapigano kutoka nchini Japani.[1] Ilianzishwa kwenye kisiwa cha Okinawa ikaenea Japani kwenye mwanzo wa karne ya 20 na kusambaa duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[2]
Karate inatumia kama silaha za mapigano pande zote za mwili kama vile mkono, ngumi, kisugudi au mguu.
Mafunzo ya karate huwa na ngazi tatu:
Kati ya michezo ya mapigano kama mchezo wa ngumi au kupiga mwereka karate inaweka mkazo kwa nguvu ya kiroho sawa na nguvu ya mwili.
Karate imefahamika duniani zaidi kutoka filamu za karate kuanzia miaka ya 1960.
Mwalimu wa karate kwa Kijapani huitwa "sensei" (kwa Kiingereza "master").