Kasi ya gimba ni umbali uliotembewa nalo kwa muda fulani. Gimba lenye kasi kubwa linapita njia kwa muda mdogo; kama kasi yake inapungua gimba litahitaji muda zaidi kwa njia hiyohiyo. Kasi ni kipimo cha mwendo wa kitu.
Katika fizikia alama ya kasi ni v (kutoka Kilatini velocitas).
Hesabu yake hufuata fomula Kasi "v" ni umbali "d" gawa kwa wakati "t":
Kuongezeka kwa kasi huitwa mchapuko (au mchapuo, kwa Kiingereza: acceleration). Kupungua kwa kasi ni mchapuohasi (kwa Kiingereza: deceleration).
Mfano: Gari linatembea kwa muda wa saa moja bila kikwazo chochote kwa mwendo usiobadilika. Kama limepita njia ya kilomita 80 katika kipindi hiki tunasema kasi ya gari ni kilomita 60 kwa saa au 60 km/h.