Katibu mkuu ni cheo cha kiongozi katika chama, shirika, kanisa, klabu au taasisi[1] . Kwa mujibu wa itifaki, yuko chini ya mkuu au mwenyekiti wa shirika, lakini mara nyingi ushawishi wake ni mkubwa kuliko wa yule ambaye ni kiongozi mkuu kwa jina. Kwa kawaida yeye ni mjumbe wa bodi kuu ya shirika, ndiye mkuu wa utawala katika shirika na mkuu wa wafanyakazi.
Kama shirika linaongozwa na kamati au bodi inayofanya maazimio ya msingi, Katibu Mkuu huwajibika kwa shughuli za kila siku.
Hata hivyo, wapo makatibu wakuu (wingi wa 'katibu mkuu') katika ngazi za serikali kama vile katibu mkuu wa baraza la mawaziri ambaye hujulikana kama katibu mkuu kiongozi hali kadhalika katibu mkuu wa wizara.[2]
Lugha ya Kiingereza ina majina kadha wa kadha kumaanisha 'katibu mkuu' kama vile secretary general, principal secretary, first secretary, executive secretary na kadhalika; tofauti na Kiswahili ambacho kina mbadala mmoja wa mtendaji mkuu.