Kaunti ya Kilifi | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
| |||||
Kilifi County in Kenya.svg Kaunti ya Kilifi katika Kenya | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 3 | ||||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani | ||||
Makao Makuu | Kilifi | ||||
Miji mingine | Malindi | ||||
Gavana | Amason Jefa Kingi | ||||
Naibu wa Gavana | Gideon Edmund Saburi | ||||
Seneta | Stewart Mwachiru Shadrach Madzayo | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Getrude Mbeyu Mwanyanje | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Kilifi | ||||
Spika | Jimmy Kahindi | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 35 | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 7 | ||||
Eneo | km2 12 539.7 (sq mi 4 841.6) | ||||
Idadi ya watu | 1,453,787 | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 116 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | kilifi.go.ke |
Kaunti ya Kilifi ni kaunti nchini Kenya katika eneo la Mkoa wa Pwani wa awali. Ilianzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha wilaya za Kilifi na Malindi.
Eneo lake ni km² 12,539.7. Eneo hilo lilikuwa na wakazi 1,453,787 wakati wa sensa ya mwaka 2019, msongamano ukiwa hivyo wa watu 116 kwa kilometa mraba[1].
Mji mkuu uko Kilifi lakini mji mkubwa zaidi ni Malindi.
Kiongozi wa serikali yake ni gavana anayechaguliwa na wananchi.
Eneo la kaunti liko upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki ya Mombasa. Sehemu zinazotembelewa na watalii ni hasa Kikambala, Watamu, Malindi na Kilifi.