Kaunti ya Kwale | |
---|---|
Kaunti | |
Kwale County in Kenya.svg Kaunti ya Kwale katika Kenya | |
Coordinates: 4°10′S 39°27′E / 4.167°S 39.450°E | |
Nchi | Kenya |
Namba | 2 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani |
Makao Makuu | Kwale |
Miji mingine | Ukunda, Mariakani, Msambweni, Lunga Lunga |
Gavana | Salim Mvurya |
Naibu wa Gavana | Fatuma Mohamed Achani |
Seneta | Issa Juma Boy |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Zuleikha Juma Hassan |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya kwale |
Spika | Sammy Ruwa |
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 |
Eneo | km2 8 267.1 (sq mi 3 191.9) |
Idadi ya watu | 866,820 |
Wiani wa idadi ya watu | 105 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | kwalecountygov.com |
Kaunti ya Kwale ni Kaunti nchini Kenya iliyoko kwenye eneo la Mkoa wa Pwani la awali. Mji mkuu uko Kwale lakini mji wake mkubwa ni Ukunda.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 eneo la kaunti lilikuwa na wakazi 866,820 katika eneo la km2 8,267.1, msongamano ukiwa hivyo wa 105 kwa kilometa mraba[1].
Kwale ina sehemu ya pwani kwenye mwambao wa Bahari Hindi kati ya Mombasa na Tanzania. Sehemu zinazotembelea sana na watalii ni Diani Beach katika tarafa ya Msambweni, Shimba Hills National Reserve na Patakatifu pa tembo pa Mwaluganje.